Meningitis; uvimbe wa utandu wa ubongo na uti mgongo ni nini?

22:45 Add Comment

 

Huu ni ugonjwa unaothiri sehemu inayofunika ubongo na uti wa mgongo, yaani utandu. Ubongo unafunikwa na sehemu au tandu tatu nyembamba za seli ili kuitengenisha na fugu la kichwa. Tandu hizi zinaweza kuathirika na kusababisha hali inayojulikana kama uvimbe wa utandu wa ubongo na uti wa mgongo.

Kwa sababu tandu zilizoathirika ziko karibu na ubongo, uvimbe wa utandu wa ubongo huwa na athari kwenye ubongo na hata kazi zake kama vile kuona, kusikia, kukumbuka, uwezo wa kutembea, uwezo wa kuzungumza na uwezo wa kukumbuka.

NI NINI HUSABABISHA UGONJWA HUU?
Aghalabu husababishwa na bacteria, lakini pia huweza kusababishwa na viumbehai kama virusi na fungi Bakteria hii hupumuliwa ndani na hupenya kupitia damu na kuathiri ubongo na uti wa mgongo. Huambukiza haraka sana/husambaa haraka sana katika maeneo ambapo kuna msongamano mkubwa na hii inaweza kugeuka kuwa mlipuko wa magonjwa.

MLIPUKO NI NINI?
Mlipuko ni ugonjwa unaoambukiza haraka na huathiri watu wengi kwa wakati mfupi sana. Mlipuko, aghalabu hutokea katika sehemu/maeneo makubwa ambapo huishi kariby sana hususan karibu na kambi za wanajeshi, kambi za wakimbizi, katika shule za bweni na kadhalika. Milipuko ya magonjwa hutokea mara moja moja miongoni mwa jamii mbalimbali/tofauti tofauti kwa wakati tufauti tofauti kwa mwaka.
NI NANI ALIYE KATIKA HATARI YA KUPATA UGONJWA HUU?
Kila mtu hupo katika hali ya hatari kuambuwa na kuugua wakati wa mlipuko/mkurupuko huu. Huambuza kirahisi na harka kutoka kwa mtu mmoja hadi mwengine.
Ilivyo kwenye magonjwa yote, ugonjwa wa utandu wa ubongo huathiri sana watoto walio chini ya miaka 5 pamoja na wakongwe. Wale walio na kinga duni k.v wale wanougua ugonjwa wa sukari, saratani, ukimwi, pia wapo katika hali ya kupata ugonjwa wa utandu wa ubongo na uti wa mgongo.

NITAJIZUIA VIPI ILI NISIPATE UGONJWA HUU?
Uzuiaji nzuri ni kupitia chanjo. Lazima watoto wote wachanjwe ili kupunguza hatari ya kuugua ugonjwa wa utandu wa ubongo.
Hata wakati wa mkurupuko wakati mwingine kuna chanjo ya kizuia maambuzi ya ugonjwa huu.
Kwa sababu ugonjwa huu huambukiza kutoka na kukaribiana kwa watu, ni muhimu kuzingatia usafi na kuwa mbali na waathiriwa wa ugonjwa wakati wa kuwatazama, kuwajulia hali ama kuwaliwaza.
Msongamano wa watu ndicho chanzo muhimu cha kuenea na kusambaa kwa ugonjwa huu kutoka kwa mtu mmoja hadi mwengine. Katika kupunguza msongamano karibu na wewe, pia unahitajika kupunguza uwezo wa kuzuia magonjwa mengine mbali na utandu wa ubongo.
NITATAMBUAJE NINAPOUGUA UGONJWA HUU? (DALILI NA ISHARA)
Ugonjwa huu huwa na joto la hali ya juu, shida ya kuona au kuepuka mwangaza, basi ni bora uende kwenye hospitali iliyo karibu nawe haraka iwezekanavyo. Hii ni muhim sana panapokuwa na mlipuko wa utandu wa ubongo na utu wa ubongo. Hii ni kwa sababu ugonjwa huu huambuza kwa kasi sana.
Usikawie ni vema kuwa na afya badala ya kujuta.

JE, KUNA TIBA YA UGONJWA HUU?
Ndiyo: huu ni ugonjwa unaosababishwa na bacteria na kuna dawa za kupambana na magonjwa yababishwayo na hewa katika hospitali zote, ambayo yanaweza kutiba ugonjwa wa utandu wa ubongo kabisa. Dawa hizi hutumiwa kupitia sindano mara nyingi kwa siku na lazima sindano hizi ziendelee kwa kipindi cha wiki/majuma mawili hadi matatu.
Iwapo kuna kukawia kufika hospitalini, dawa hiyo haiwezi kusaidia kutibu mgonjwa ambaye amezidiwa na ugonjwa huu. Haitafanya kazi kwa vyovyote vile. Kwa hivyo ni muhimu kuenda hospitalini kwa wakati unaofaa dalili zinapoonekana.
KUTAKUWA NA UBAYA GANI IWAPO SIPATI MSAADA? (MATATIZO)
Ugonjwa wa utandu wa ubongo huambukiza haraka na kwa sababu ni hatari, husabisha kifo iwapo hautibiwi. Wagonjwa wote wa utandu wa ubongo lazima walazwe hospitalini kwa sababu huzingatiwa kuwa dharura ya kimatibabu. Aghalabu, hili hujiri mgonjwa anapoenda hospitalini akichelewa ili kupata matibabu.
Madhara hufungamana na utendakazi wa ukongo na huhusisha upofu, usiwi na kutoweza kutumia mikono na miguu vizuri, kutozungumza kwa ufasaha and nafuu siyo nzuri.

NITAMTUNZA VIPI MTU AMBAYE ANAUGUA UGONJWA HUU (UTANZAJI WA NYUMBANI)?
Haushauriwi kumtunzia mgonjwa wa utandu wa ubongo nyumbani. Hii ni dharura ya kimatibabu inayostahili kutatuliwa hospitalini kati ya wiki 2-3. Iwapo unashuku kwamba Fulani wanaugua ugonjwa huu, wapeleke hospitalini haraka iwezekanavyo.
Wanapokuwa kwenya matibabu na sasa wamerudi nyumbani, husalia kuwa wanyonge. Kwa Hivyo vema kwao kutunzwa. Sharti chakula chao kiwe chepesi chenye na virutubishi wape kiasi kidogo kila baada ya saa mbili. Hii ni kwa sababu hamu yao ya chakula imerudi chini. Watie moyo wagonjwa ambao wana madhara kutokana na ugonjwa huu.
HOJA MUHIMU KUHUSU UGONJWA WA UTANDU WA UBONGO
·         Utandu ni ugonjwa wa ubongo na uti wa mgongo unaotibika. Husambaa haraka sana katika maeneo palipona msongamano na iwapo hautatibiwa.
·         Huathiri sana sana watoto an wakongwe lakini wakati wa mlipuko/mkumpuko huathiri vijana wanaume na wanawake wape watoto kinga kupitia chanjo.
·         Dalili za ugonjwa wa utandu, joto la hali ya juu, kutapika, kuumwa kichwa na kuepuka mwangaza. Kupitia kwa shingo huwa dalili ya mwisho. Watoto walio chini ya miaka 2 wanaweza kuwa na joto tu pamoja na kulia.
·         Ugonjwa wa utandu unaweza kuua kati ya saa au siku chache. Iwapo unaushuku, mkimbize mtoto au mtu mzima hospitalini kwa ajili ya kupimwa. Wanaweza kulazwa kwa ajili ya matibabu.

Ugonjwa Wa Kifua kikuu (tb)

15:05 Add Comment

Kifua kikuu ni ugonjwa unaosababishwa na vimelea vya bacteria na kuenezwa kwa njia ya hewa. Mtu mwenye maambukizi ya kifua kifua kikuu akikohoa,
kupiga chafya au kutema mate ovyo husambaza vijidudu hivyo hewa, huweza kumwabukiza mtu mwingine kama atakuwa hajaanza kutumia dozi ya kifua kikuu.

DALILI ZA KIFUA KIKUU (TB)
  • Kukohoa kwa muda wa wiki mbili au zaidi
  • Maumivu ya kifua
  • Homa za usiku
  • Kutoka jasho kwa wingi usiku
  • Kupungua uzito
  • Kukohoa damu
  • Kukosa hamu ya chakula na mwili kuwa dhaifu

ATHARI ZA KIFUA KIKUU (TB)
  • Ugonjwa huweza kuenea kwenye viungo vingine vya mwili
  • Watu wengine hupoteza maisha iwapo hawatapata tiba sahihi mapema
  • Watu wengine huambukizwa ugonjwa katika muda mfupi
  • Wagonjwa wa kifua kikuu hawazezi kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendelea
  • Matibabu ya kifua kikuu huchua muda mrefu na ni gharama kubwa
KINGA

Ugonjwa huu unakingwa kwa chanjo ya kifua kikuu kwa kitaalamu (BCG) ambayo hutolewa mara tu motto anapozaliwa.
Ili kupunguza uwezekano wa kupata kifua kikuu zingatia yafuatayo;
  • Kujenga na kuishi kwenye nyumba zinazoruhusu mzunguko kwa hewa ya kutosha (ziwe na madirisha makubwa ya kutosha)
  • Epuka kukaa kwenye msongamano wa watu wengi
  • Watoto wanyonyeshwe maziwa ya mama pekee kwa miezi sita na umlikiza kwa vyakula vyenye virutubisho ili kumjengea kinga imara
  • Kula vyakula vyenye lishe bora
  • Kutotema mate na makohozi ovyo ili kuziua usambaaji wa bacteria wasababishao Kifua kikuu.

 RATIBA YA CHANJO
Chanjo ya kifua kikuu hutolewa baada ya motto kuzaliwa au anapofika kliniki kwa mara ya kwanza
Iwapo kovu kwa motto halijajitokeza chanjo irudiwe katika kipindi cha miezi 3.


TIBA YA KIFUA KIKUU (TB)
Ugonjwa wa kifua kikuu unatibika.
Matibabu yake huchukua muda mrefu wa miezi 6 hadi 8 na ni ya gharama kubwa.
Inashauriwa mgonjwa awahi matibabu mapema kwenye vituo vya kutolewa huduma za kinga.

UJUMBE
  • Ugonjwa wa kifua kikuu ni hatari, hata hivyo unakingwa kwa chanjo.
  • Mzazi au mlezi hakikisha kila motto anapozaliwa anapata chanjo ya kuzuia kifua kii 

“Kumbuka chanjo ya kifua kikuu (BCG) Itamkinga mtoto dhidi ya ugonjwa wa kifua kikuu”

Madhara ya unene uliopitiliza (obesity)

09:33 Add Comment

Tatizo hili la unene uliopitiliza kuliko inavyo hitajika kiafya huwa linaletwa na kuongezeka kwa kiwango cha mafuta mwilini.
Njia rahisi na inayokubalika ya kuweza kugundua kama mtu ni mnene kupita kiasi (obese) inafahamika kama kipimo cha Body Mass Index (BMI).










 Vipimo hivi vya BMI ndio vinaweza kukujulisha kama unene ulionao unastahili kulingana na umri, urefu na uzito wako. Vipimo hivi ni kama ifuatavyo:
Jinsi ya kupima BMI yako
Kanuni ya BMI hutumia uzito wa mtu pamoja na urefu wake. Uzito wa mtu hupimwa katika kilograms (kg) na urefu wake katika mita (m) au sentimita (cm). Ikumbukwe pia kuwa mita moja ni sawa na sentimita 100 na mita² = mita x mita.

 BMI (kg/m2) = Uzito katika kilograms/Urefu katika meters². Maana yake ni kwamba ili kuweza kupata BMI itakayokuwezesha kujifahamu kama u mnene ama la, chukua uzito wako gawa kwa kipeo cha pili cha urefu wako.
Tatizo la unene uliopitiliza husababishwa na nini ?
Kuna mambo kadhaa yanayoweza kusababisha unene uliopitiliza. Mambo hayo ni pamoja na
v  Vyakula vya mafuta - Ulaji wa vyakula venye mafuta mengi au calories nyingi.
v  Kutofanya mazoezi - Wale wasiofanya mazoezi mara kwa mara huwa wanene tofauti na wale wanaofanya mazoezi.
v  Kurithi viashiria vya asili (genes) - Viashiria hivi vinaweza kuwa moja ya vichocheo vya kuongeza uzito kwani ndivyo huamua wapi mafuta huhifadhiwa mwilini na kwa kiwango gani. Lakini haimanishi kuwa mtu akiwa navyo basi ndio atakumbwa na tatizo hili.
v  Umri - Watu wengi huongezeka uzito au hunenepa kadri umri unavyoongezeka kwa sababu wanakuwa hawajishughulishi sana (less active) na huwa wanapungua maumbile ya miili yao (muscles mass)
v  Matatizo ya kisaikolojia - Wakati mwengine watu wenye matatizo ya kisaikolojia au msongo wa mawazo (stress) huwa na tabia ya kula sana, matokeo yake ni kunenepa.
v  Dawa - Baadhi ya dawa zenye madhara ya kuongeza unene ni kama corticosteroids, blood pressure medications, tricyclic medications na kadhalika.
v  Matatizo ya afya - Baadhi ya magonjwa yanachangia kuongezeka kwa uzito au kenenepa kama cushings syndrome, hypothyroidism, osteoarthritis na kadhalika

Vihatarishi vya tatizo la unene wa kupitiliza
Aidha yapo mambo kadhaa ambayo yanaweza kumuhatarisha mtu kupata unene wa kupitiliza. Mambo haya ni pamoja na
v  Kukua kwa uchumi wa nchi - Wananchi wengi wanaoishi kwenye nchi zilizoendelea au wenye kipato kikubwa ndio wanaopata tatizo hili kutokana na kuishi mfumo wa maisha ya kivivu na hali ya kutokufanya mazoezi (sedentary lifestyle).
v  Historia ya kuongezeka uzito uliopitiliza kwenye familia nayo yaweza kuhatarisha mtu kupata tatizo hili. Aidha, si jambo la kushangaza kuona karibu familia nzima au wengi wa wanafamilia kuwa wanene kupitiliza.
v  Kutojishughulisha na chochote (inactive).
v  Kupenda kula sana kuliko kawaida (overeating).
v  Kula vyakula vya mafuta mengi
v  Kutumia dawa zenye madhara ya kuongeza uzito uliopitiliza.
v  Kuwa na ugonjwa wa vichocheo mwilini (hormonal disorders) kama cushing syndrome, hypothyroidism.
v  Kuwa na msongo wa mawazo au kuathirika kisaikolojia.

 Magonjwa yanaoweza kuambatana na tatizo la unene uliopitiliza
Ø  Kisukari
Ø  Shinikizo la damu (hypertension)
Ø  Kiharusi (Stroke)
Ø  Magonjwa ya moyo
Ø  Tatizo la kutopumua vizuri wakati mtu yupo usingizini (Sleep apnea)
Ø  Vijiwe katika mfuko wa nyongo (Gallstones)
Ø  Kiwango cha juu cha lijamu kwenye damu (cholesterol ikiwemo triglycerides)
Ø  Ugonjwa wa mifupa kama yabisi (osteoarthritis).
Ø  Saratani ya matiti
Ø  Saratani ya tezi dume (prostate cancer)
Ø  Saratani ya utumbo mpana pamoja na maeneo ya haja kubwa (Colorectal cancer)
Ø  Matatizo ya mzunguko na mishipa ya damu kama vile kuvimba kwa vena za miguuni (varicose veins)


Tiba ya kuongezeka unene kupita kiasi
Tiba ya tatizo hili ni mhusika kujitambua ya kwamba ana tatizo na kuwa tayari kupunguza uzito. Mabadiliko ya tabia ya mhusika ni muhimu sana, mabidiliko haya yawe ndio mfumo wa maisha yake ya kila siku.
Kupungua uzito na kujilinda au kutunza uzito ulionao baada ya kupunguza uzito ni jambo la msingi sana na inahusisha mazoezi, chakula na madiliko ya tabia ya mtu.
·         Mabadiliko ya tabia - Hii inahusisha muhusika kupunguza kiwango cha chakula anachokula lakini kiwe chenye virutubisho vyote muhimu vya afya na kuongeza kiwango cha ufanyaji mazoezi.
·         Mazoezi - Mazoezi husaidia kupunguza uzito hasa kipindi cha miezi sita ya mwanzo na hutunza uzito uliokusudiwa kwa muda mrefu. Pia hupunguza mafuta ya mwilini, huongeza ufanisi wa moyo, hupunguza tatizo la shinikizo la damu (hypertension), na kuweka sukari katika kiwango kinachohitajika mwilini.
Kama hujazoea kufanya mazoezi ni vizuri uanze taratibu na ujiwekee lengo kwa kufanya mazoezi kwa muda wa nusu saa kila siku, siku tano kwa wiki,(dakika 30 kila siku kwa siku tano kwa wiki). Mazoezi mazuri ni kama kuogelea, kuendesha baiskeli, kutembea, kunyanyua vitu vizito (visiwe vyenye uzito mkubwa), mazoezi ya viungo na kadhalika. Kama mtu ni mnene sana basi ni bora kuzungumza na daktari wako kabla ya kuanza mazoezi mapya. Baada ya kuanza mazoezi kwa mara ya kwanza, mwili utakuwa na maumivu, hii ni kawaida lakini kama mtu atapata maumivu zaidi ya masaa 2 baada ya kufanya mazoezi ni vizuri kumuona daktari.
·         Dawa - Zipo dawa nyingi za kupunguza uzito lakini ikumbukwe ya kwamba hakuna tiba ya tatizo hili na dawa hizi zina madhara mengi kama kuongeza shinikizo la damu (hypertension), matatizo ya moyo, kuharisha,msongo wa mawazo (depression) na mengineyo.
·         Chakula - Msingi wa kupunguza uzito au unene ni kujua ni kiwango gani cha calories mwili wako unahitaji kwa siku ili uwe unakula chakula ambacho hakitazidisha au kupunguza kiwango cha calories unazohitaji kwa siku. Mlo mzuri ni ule ulio na matunda kwa wingi, mboga za majani, nafaka ambazo hazijakobolewa, mafuta kidogo (less saturated fat). Vyakula vengine ni kama mayai, nyama isiokuwa ya mafuta (lean meat), samaki, kuku na vingineyo.

·         Tiba ya upasuaji - Kuna aina nyingi za upasuaji ambao unasaidia kupunguza uzito aina hizi ni kama gastric banding, gastric bypass (Roux-en-Y-procedure), liposuction. Kabla ya kufanyiwa upasuaji, muhusika atahitaji kupimwa kisaikolojia (psychological testing) na kupewa ushauri nasaha kwani tiba hii pia ina madhara yake.

 Wanawake ambao wana uzito wa kupitiliza (obese women) wakiwa wajawazito wako kwenye hatari ya kupata madhara yafuatayo;
·         Kisukari cha mimba (Gestatitional diabetes) - kisukari hiki kinatokea wakati wa ujauzito na hupotea baada ya kujifungua mtoto.
·         Shinikizo la damu (hypertension)
·         Shinikizo la damu wakati wa ujauzito pamoja na kifafa cha mimba (pre-eclampsia & eclampsia)
·         Kuzaa kwa njia ya upasuaji (caesarean section)
·         Tatizo la kiumbe kutopata hewa vizuri wakati wa ujauzito (fetal distress)

Kutoka Mimba

12:26 Add Comment

Tatizo la mimba kutoka au kutolewa ni jambo ambalo limewakumba kina mama wengi walio katika umri wa kuzaa. Aidha mijadala kuhusu kuhalalishwa au kuendelea
kuharamishwa kwa utoaji mimba ni jambo linalochukua nafasi ya mazungumzo ya kila siku katika maisha yetu.

Kwa baadhi ya nchi, suala la utoaji mimba ni jambo lililohalallshwa kisheria ingawa kwa nchi kama Tanzania, suala hili halijahalalishwa isipokuwa tu pale panapokuwa na sababu za kitabibu zinazolazimisha kufanya hivyo.

Nini maana ya mimba kutoka (abortion)
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), utokaji mimba (abortion) hutokea pale ambapo kiumbe (mimba) kilicho chini ya wiki 22 kinapotoka kwa sababu moja ama nyingine, au kinapotolewa kwa njia yeyote ile. Aidha shirika la Afya limekwenda mbali zaidi na kutoa maana nyingine ya utokaji mimba kuwa ni pale mtoto (kiumbe) anapozaliwa akiwa na uzito wa chini ya gram 500.

Aidha baadhi ya matabibu hupendelea kutumia neno 'abortion' kumaanisha kitendo cha utoaji wa mimba kinachofanywa na mtu mwingine ama kwa njia sahihi au zisizo sahihi na 'miscarriage' kumaanisha kitendo cha mimba kutoka yenyewe kwa sababu nyingine yeyote. Ukiacha tofauti hizi za jinsi ya kuharibika kwa mimba, abortion na miscarriage humanisha kitu kilekile cha mimba kutoka.

 Aina za utokaji/utoaji mimba (Classification of abortion)
Utokaji mimba umeanishwa katika aina zifuatazo

  1.     Utokaji wa mimba wa hiyari yaani kitendo cha mimba kutoka yenyewe (spontaneous abortion)
  2.     Mimba inayotishia kutoka ingawa bado haijatoka (threatened abortion)
  3.     Utokaji wa mimba usioepukika (inevitable abortion)
  4.     Utokaji wa mimba ulio kamili (complete abortion)
  5.     Utokaji wa mimba usio kamili (incomplete abortion)
  6.     Mimba iliyotoka bila kugundulika kuwa imetoka (missed abortion)
  7.     Utokaji wa mimba unaojirudia rudia (recurrent abortion)
  8.     Utoaji mimba kinyume cha sheria (illegal abortion)
  9.     Utoaji mimba kwa sababu za kiafya (therapeutic abortion)
 1. Utokaji mimba kwa hiari au kitendo cha mimba kutoka yenyewe (spontaneous abortion)

Hii ni hali inayotokea pale mimba inapoharibika na kutoka bila kuwepo kwa sababu yeyote iliyo dhahiri, kwa maana nyingine mimba uharibika na kujitokea bila kusababishwa na mtu wala kitu chochote.
Utokaji mimba wa namna hii umegawanyika katika aina kuu nne ambazo ni
1.   Mimba inayotishia kutoka ingawa bado haijatoka (threatened abortion)
2.   Mimba isiyoepukika kutoka (Inevitable abortion)
3.   Mimba inayotoka yote au kamili (complete abortion), na
4.   Utokaji mimba usio kamili (Incomplete abortion)

Mimba inayotishia kutoka (threatened Abortion)
Tatizo hili hutokea mapema wakati wa ujauzito. Hali hii hujionesha kwa damu kutoka ukeni wakati njia ya shingo ya uzazi ikiwa bado imefunga. Mara nyingi mimba inayotishia kutoka haina tabia ya kuambatana na maumivu yeyote ya tumbo.

Daktari anapompima mgonjwa hukuta shingo ya kizazi ikiwa imefunga na hakuna dalili zozote za kiumbe kutoka ingawa mgonjwa hutokwa na damu sehemu za siri. Aidha mgonjwa huwa hana maumivu yeyote ya tumbo.
Mimba isiyoepukika kutoka (inevitable abortion)
Hii ni hali inayotokea mapema wakati wa ujauzito pale damu inapotoka ukeni wakati njia ya shingo ya kizazi ikiwa imefunguka au kuwa wazi. Aidha, kwa kawaida, kiasi cha damu kinachotoka ni kingi na mgonjwa hujisikia maumivu makali sana ya tumbo.
Utokaji mimba usioepukika waweza kupelekea

·       Utokaji mimba ulio kamili (complete abortion), au
·       Utokaji mimba usio kamili (incomplete abortion).
·       Utokaji mimba usio kamili (incomplete abortion)
·       Utokaji mimba usio kamili huambatana na utokaji damu kwa wingi

sehemu za siri za mgonjwa, kufunguka kwa njia ya shingo ya kizazi, kutoka kwa baadhi ya mabaki ya kiumbe (products of conception) ingawa mengine hubakia, na mgonjwa kujisikia maumivu makali ya tumbo hususani sehemu za chini ya kitovu.

Utokaji wa mimba ulio kamili (complete abortion)
Hali hii huambatana na mama kutokwa damu sehemu za siri, kujisikia maumivu makali ya tumbo pamoja na kutoka kwa kiumbe ikiambatana na kondo lake la nyuma. Aidha baada ya muda, mgonjwa hueleza kupotea kwa maumivu ya tumbo, damu kupungua kutoka sehemu za siri na kufunga kwa njia ya njia ya shingo ya kizazi (cervix).

Mimba iliyotoka bila kugundulika kuwa imetoka (missed abortion)
Hali hii hutokea pale ambapo, kiumbe kinapokuwa kimekufa bila ya mimba kutoka. Mara nyingi, damu huwa haitoki sehemu za siri, na mgonjwa huwa hajisikii maumivu yeyote ya tumbo. Aidha huwa hakuna dalili zozote za ukuaji wa mimba na hata mapigo ya moyo ya mtoto hayawezi kutambulika hata kama vipimo maalum vitatumika.

Utokaji wa mimba unaojirudia rudia (recurrent abortion)
Hali hii hutokea pale ambapo mama huwa na historia ya mimba kutoka mara tatu au zaidi kwa mfululizo.
Utoaji mimba kinyume cha sheria (illegal abortion)
Utoaji mimba kinyume cha sheria ni usitishwaji wa maisha ya mimba au kutolewa kwa kiumbe kinyume na sheria za nchi husika zinavyoagiza. Katika mazingira kama haya, sababu dhahiri za kitaalamu hukosekana isipokuwa wahusika hutenda kulingana na sababu zao binafsi zikiwemo za kutoitaka mimba au kama ni muhusika ni mwanafunzi huogopa kufukuzwa shule.

 Utoaji mimba kisheria kwa sababu za kitabibu (therapeutic abortion)
Utoaji mimba ulioidhinishwa kitabibu ni usitishwaji wa mimba kwa ajili ya kuokoa maisha ya mama. Usitishwaji huu ni hufanywa kitaalamu na daktari. Sababu zinazoweza kufanya mimba ikasitishwa ni pamoja na

·       iwapo kiumbe kina mapungufu mengi ya kimaumbile (fetal anomally) ambayo yatamletea mtoto atakayezaliwa matatizo na hata kusababisha kifo chake
·       iwapo mama mjamzito alipata ujauzito kwa kubakwa na asingependa kuzaa, au
·       iwapo mama mjamzito ana kansa , kwa mfano, kansa ya kiwanda cha mayai ya kike (ovarian cancer), kansa ya damu (leukemia) au kansa ya tezi la goita (thyroid cancer)
·       Mambo gani hufanya mimba kutoka kwa hiyari?
·       Kuna sababu kadhaa zinazoweza kupelekea mimba kutoka kwa hiyari (spontaneous abortion). Miongoni mwa sababu hizo ni
·       Matatizo kwenye mfumo wa jenetiki (genetic abnormalities) ambayo husababisha kuharibika na kutoka kwa mimba katika miezi mitatu ya mwanzoni.
·       Matatizo kwenye mfuko wa uzazi (uterine problems): matatizo kama vile kuwepo kwa uvimbe kwenye mfuko wa uzazi wa mwanamke (uterine fibroids), au kulegea kwa milango ya shingo ya kizazi (cervical incompetence)husababisha mimba kutoka katika theluthi ya pili ya ujauzito (second trimester).
·       Sababu nyingine ni pamoja na maradhi wakati wa ujauzito kama malaria, kisukari, shinikizo la damu, kifafa cha mimba, matatizo kwenye tezi ya 'goita' (hypothyroidism). Aidha maambukizi kama Rubella, toxoplasmosis na mengineyo nayo pia huweza kusababisha mimba kutoka.
·       Kukosekana kwa ulinganifu katika baadhi ya homoni mwilini (hormonal imbalance)
·       Matumizi ya baadhi madawa kwa mfano zinazotumika katika kutibu msongo wa mawazo kama vile paroxetine auvenlafaxine nayo yaweza kusababisha utokaji wa mimba.
·       Tabia hatarishi zinazoweza kusababisha utokaji wa mimba
·       Unywaji pombe uliopitiliza.
·       Uvutaji sigara
·       Utumiaji madawa ya kulevya kama vile kokeini (cocaine)
·       Utumiaji kwa wingi wa vinywaji vyenye kiasili cha caffeine kama vile kahawa au kakao.
·       Vipimo na Uchunguzi
·       Ili kutambua kuwepo kwa hali hii ya mimba kutoka, vipimo vifuatavyo vyaweza kufanywa na tabibu
·       Kipimo cha mimba kwa kutumia mkojo (Urine for hCG)
·       Kupima damu ili kufahamu kiasi cha wingi wa damu (haemoglobin level), kundi la damu (blood group) na muda wa damu kuganda (bleeding and clotting time).
·       Kuchunguza iwapo shingo ya uzazi imefunga au ipo wazi, na pia kuchunguza iwapo kuna dalili ya kiumbe kutoka ama la. Uchunguzi huu huitwa speculum examination.
·       Ultrasound ya nyonga (pelvic utrasound) kwa ajili ya kutambua iwapo kiumbe kipo ama la, na kama kipo je ki hai ama kimekufa.
·       Aidha ni muhimu pia kufanya uchunguzi wa magonjwa mbali ya zinaa ambayo husababisha mimba kutoka.

Matibabu ya utokaji wa mimba
Matibabu ya utokaji wa mimba hutegea sana aina ya utokaji wa mimba. Hata hivyo, ni muhimu kuzingatia vitu vifuatavyo wakati wa kutoa matibabu kwa mtu aliyepoteza mimba
Wahudumu wa afya huzingatia kanuni zote (ABC) za kuokoa maisha ya mgonjwa kama vile
·         kuhakikisha njia ya hewa ya mgonjwa ipo wazi na hewa inaingia na kutoka vizuri kwenye mapafu
·         kuhakikisha mgonjwa anapumua vizuri bila shida
·         kuhakikisha mishipa ya damu ya mgonjwa imewekwa mrija wa veni (intravenous line) na mgonjwa anapewa dripu ya maji ya normal saline.
·         kuhakikisha mgonjwa anaongezwa damu haraka iwapo vipimo vitaonesha kuwa alipoteza damu kwa wingi
Matibabu ya mimba inayotishia kutoka (threatened abortion)
Kwenye hali hii, mgonjwa hutakiwa            
·         kupumzika kitandani bila kufanya kazi yeyote (complete bed rest) angalau kwa wiki moja au zaidi mpaka hapo damu itakapoacha kabisa kutoka
·         kumpa ushauri na uhakika mama ili kumfanya atulie kiakili (assurance and proper councelling)
·         Mama pia hupewa dawa za kumtuliza na kumfanya apumzike (sedatives) kama vile phernobabitone
·         Aidha mama hupewa dawa kwa ajili ya kupunguza kusukuma kwa uterus (antispamodics) kama vile salbutamol
·         Kutofanya tendo la ndoa kwa wiki mbili au tatu
·         Aidha mama na mumewe hupewa ushauri juu ya tatizo hilo na jinsi ya kuendelea na matibabu
Matibabu ya mimba iliyotoka kamili (complete abortion)

Mara nyingi mgonjwa huwa haitaji matibabu zaidi ya uangalizi wa karibu kwa vile kiumbe pamoja na kondo lake la nyuma vyote huwa vimetoka kikamilifu. Mara chache sana, kulingana na jinsi daktari atakavyoona, mgonjwa anaweza kupewa antibiotiki kwa ajili ya kuzuia uwezekano wa kupata maambukizi.

Matibabu ya utokaji wa mimba usiokuwa kamili (incomplete abortion)
Matibabu ya aina hii ya utokaji wa mimba uhitaji mgonjwa kusafishwa kwa ajili ya kuondoa mabaki ya kiumbe (products of conception) yaliyobakia. Usafishaji huu huweza kufanywa kwa kutumia njia inayoitwa Manual Vacuum Aspiration (MVA).

Aidha mgonjwa hupewa dawa za antibiotiki kwa ajili ya kuzuia uwezekano wa maambukizi ya vimelea vya bakteria. Matibabu mimba iliyotoka bila kugundulika kuwa imetoka (missed abortion)

Matibabu ya aina hii ya utokaji wa mimba ni pamoja na mgonjwa kuwekewa maji ya uchungu ili kiumbe kiweze kutoka. Wakati mwingine, daktari anaweza kuamua kusafisha mfuko wa uzazi (uterus) kwa kutumia njia inayoitwa dilatation and curettage. Sambamba na matibabu hayo, mgonjwa pia hupewa dawa za antibiotiki kwa ajili ya kuzuia maambukizi ya vimelea vya bakteria.

Matibabu ya tatizo la utokaji wa mimba unaojirudia (recurrent abortion)
Jambo la msingi katika matibabu ya tatizo la utokaji mimba unaojirudia (recurrent abortion) ni kugundua na kutambua chanzo kinachosababisha tatizo hilo na kisha kukishughulikia ili kuondoa kabisa kujirudia rudia kwa tatizo hili.

·    Kuchunguza iwapo shingo ya uzazi imefunga au ipo wazi, na pia kuchunguza iwapo kuna dalili ya kiumbe kutoka ama la. Uchunguzi huu huitwa speculum examination.
·   Ultrasound ya nyonga (pelvic utrasound) kwa ajili ya kutambua iwapo kiumbe kipo ama la, na kama kipo je ki hai ama kimekufa.
· Aidha ni muhimu pia kufanya uchunguzi wa magonjwa mbali ya zinaa ambayo husababisha mimba kutoka.
Matibabu ya utokaji wa mimba
Matibabu ya utokaji wa mimba hutegea sana aina ya utokaji wa mimba. Hata hivyo, ni muhimu kuzingatia vitu vifuatavyo wakati wa kutoa matibabu kwa mtu aliyepoteza mimba
Wahudumu wa afya huzingatia kanuni zote (ABC) za kuokoa maisha ya mgonjwa kama vile
· kuhakikisha njia ya hewa ya mgonjwa ipo wazi na hewa inaingia na kutoka vizuri kwenye mapafu
·    kuhakikisha mgonjwa anapumua vizuri bila shida
·         kuhakikisha mishipa ya damu ya mgonjwa imewekwa mrija wa veni (intravenous line) na mgonjwa anapewa dripu ya maji ya normal saline.
·         kuhakikisha mgonjwa anaongezwa damu haraka iwapo vipimo vitaonesha kuwa alipoteza damu kwa wingi
Matibabu ya mimba inayotishia kutoka (threatened abortion)
Kwenye hali hii, mgonjwa hutakiwa            
kupumzika kitandani bila kufanya kazi yeyote (complete bed rest) angalau kwa wiki moja au zaidi mpaka hapo damu itakapoacha kabisa kutoka
kumpa ushauri na uhakika mama ili kumfanya atulie kiakili (assurance and proper councelling)
 Mama pia hupewa dawa za kumtuliza na kumfanya apumzike (sedatives) kama vile phernobabitone
 Aidha mama hupewa dawa kwa ajili ya kupunguza kusukuma kwa uterus (antispamodics) kama vile salbutamol
 Kutofanya tendo la ndoa kwa wiki mbili au tatu
 Aidha mama na mumewe hupewa ushauri juu ya tatizo hilo na jinsi ya kuendelea na matibabu
Matibabu ya mimba iliyotoka kamili (complete abortion)

Mara nyingi mgonjwa huwa haitaji matibabu zaidi ya uangalizi wa karibu kwa vile kiumbe pamoja na kondo lake la nyuma vyote huwa vimetoka kikamilifu. Mara chache sana, kulingana na jinsi daktari atakavyoona, mgonjwa anaweza kupewa antibiotiki kwa ajili ya kuzuia uwezekano wa kupata maambukizi.
Matibabu ya utokaji wa mimba usiokuwa kamili (incomplete abortion)
Matibabu ya aina hii ya utokaji wa mimba uhitaji mgonjwa kusafishwa kwa ajili ya kuondoa mabaki ya kiumbe (products of conception) yaliyobakia. Usafishaji huu huweza kufanywa kwa kutumia njia inayoitwa Manual Vacuum Aspiration (MVA).
Aidha mgonjwa hupewa dawa za antibiotiki kwa ajili ya kuzuia uwezekano wa maambukizi ya vimelea vya bakteria.

Matibabu mimba iliyotoka bila kugundulika kuwa imetoka (missed abortion)
Matibabu ya aina hii ya utokaji wa mimba ni pamoja na mgonjwa kuwekewa maji ya uchungu ili kiumbe kiweze kutoka. Wakati mwingine, daktari anaweza kuamua kusafisha mfuko wa uzazi (uterus) kwa kutumia njia inayoitwa dilatation and curettage. Sambamba na matibabu hayo, mgonjwa pia hupewa dawa za antibiotiki kwa ajili ya kuzuia maambukizi ya vimelea vya bakteria.

Matibabu ya tatizo la utokaji wa mimba unaojirudia (recurrent abortion)
Jambo la msingi katika matibabu ya tatizo la utokaji mimba unaojirudia (recurrent abortion) ni kugundua na kutambua chanzo kinachosababisha tatizo hilo na kisha kukishughulikia ili kuondoa kabisa kujirudia rudia kwa tatizo hili.

Mambo ya kuzingatia kabla ya kutoboa/kuchorwa (tattoo) mwili

19:47 Add Comment
Zamani ilikuwa ni kawaida kuona wanawake wanatoboa  masikio, pua, ili kuvaa aina mbalimbali za herini na shemeri. Siku hizi si ajabu kuona wanaume na wanawake wakijitoboa au kuchorwa alama (tattoo)
sehemu mbalimbali za miili yao kama kwenye pua, mdomo, ulimi, tumbo, masikio, mikono, miguu, kwenye kichwa, mapaja, mgongo  na hata sehemu za siri yote haya kwa ajili ya urembo, miila au desturi zao, kutaka kujinasibu na tabaka fulani au kutaka kuonyesha ubunifu wao(artistic expression).

Kutoboa/kuchorwa mwili kama kutafanywa na mtaalamu wa kutoboa/kuchora mwili hakuna madhara yoyote ya kiafya, madhara ya kutoboa/kuchorwa mwili  hupatikana pale tu ambapo kitendo hiki  hufanywa na mtu ambaye si mtaalamu na mjuzi wa fani hii bila kutumia njia salama za kiafya.

Katika utafiti uliofanywa nchini Marekani na madaktari bingwa wa ngozi (dermatologists) katika chuo kikuu chaNorthwestern University Feinberg School of Medicine na kuchapishwa katika jarida la   American Journal of Clinical Dermatology umesema tatizo kubwa la kutoboa/kuchorwa mwili ni maambukizi (infection) yanayokisiwa kufika asilimia 20 ya kutoboa/kuchorwa sehemu mbalimbali za mwili. Maambukizi haya mara nyingi husababishwa na bakteria na huonekana katika sehemu ya mwili iliyotobolewa/kuchorwa.Madhara mengine ya kutoboa/kuchorwa mwili ni kuvuja damu, mzio/aleji, ngozi kuchanika pamoja  na ngozi kuwa na baka au scarring.

Ni mambo gani ya kuzingatia kabla ya kutoboa/kuchorwa  mwili wako?
1.Unatakiwa kujua  uwezekano wako wa kupata maambukizi - Kama tayari una maambukizi au una kidonda kilichowazi, ni bora ukaacha kutoboa/kuchorwa mwili mpaka utakapopona na kuwa na afya njema. Hatari ya kupata maambukizi ni kubwa kama utatobolewa/kuchorwa na mtu ambaye si mtaalamu na hana ujuzi wa kufanya kazi hii. Hakikisha anayekufanyia  hivi awe anafahamu masuala ya kukinga wateja wake na maambukizi ambayo ni pamoja na kusafisha vifaa vyake kila baada ya kazi, kuvichemsha vifaa hivyo au kuhakikisha vipo salama na havina bakteria wowote kwa kutumia kemikali za kusafishia, kuvifunika vifaa hivyo baada ya kuvisafisha na yeye mwenyewe kuvaa gloves salama(surgical gloves) wakati wa kufanya kazi yake hiyo ili hata kama ana magonjwa ya kuambukiza asiweze kukuambukiza wewe kwani zipo taarifa ambazo watu wameambukizwa ugonjwa wa ukimwi  au wamepata ugonjwa wa tetanus wakati wa kutobolewa/kuchorwa miili yao.

2.Hakikisha huna maradhi yoyote sugu - Kama una maradhi ya kisukari, ni bora ukaepuka kutoboa/kuchorwa mwili kwani kidonda chake kinaweza kisipone haraka na hatari ya maambukizi kwa wagonjwa wa sukari iko juu kupitia kwenye vidonda.

3.Fahamu kuhusu uwezo wako wa kupona - Unatakiwa uwe na ufahamu juu ya uwezo wa mwili wako katika kupona(healing tendencies) kidonda chochote kile. Kuna watu wengine wanapopata mchubuko au kukatika ngozi zao hupona kwa ngozi ile kufanya kama baka na uvimbe unaojulikana kama keloids. Kama wewe ni mmoja wa watu wa aina hii basi unahitaji kuepuka kufanya kitendo hiki cha kutoboa/kuchora mwili wako. Sehemu ambazo huchukua muda mrefu kupona baada ya kutoboa/kuchora mwili ni pamoja na kwenye maeneo ya tumboni, kwenye chuchu na hata sehemu za siri kwa wanawake.

4.Jua maumbile yako-Sio kila ngozi ya mwanadamu inafaa kwenye kuitoboa/kuchora, mfano, wale wenye ngozi  ya kwenye tumbo iliyoenuka ndio hufaa kutoboa sehemu hii, kama unataka kutoga ulimi na ulimi huo ni mfupi kutokana na umbile lako, (Tongue with short frenum) yaani wale wenye mkunjo chini ya ndimi zao  na hivyo kufanya ulimi kuwa mfupi, hawapaswi kutoga ndimi zao.

5.Hakikisha unafanyiwa na mtaalamu wa fani hii.Wataalamu wa mambo ya kutoboa/kuchora mwili wana uelewa mkubwa wa maumbile ya mwanadamu na huwa na vifaa vya kuzuia uvujaji wa damu pindi unapotokea. Pia huwa na ufahamu wa jinsi ya kukulinda na maambukizi .

6.Historia yako ya afya- Wataalamu wa kutoboa/kuchora mwili wanatakiwa kuchukua historia ya  afya ya wateja wao inayohusisha magonjwa ya moyo, ugonjwa wa kisukari, mzio/aleji, ugonjwa wa pumu na kadhalika. Kama unatumia dawa za ugonjwa wowote ule ni bora ukamweleza mapema mtaalamu huyo kabla hajaanza kukutoboa/kukuchora mwili wako. Ili kuzuia uvujaji wa damu kwa wingi, unashauriwa kuepuka dawa aina ya aspirin angalau kwa wiki moja kabla ya kutoboa/kuchora mwili  wako, pia epuka dawa jamii ya Non Steroidal Anti-Inflammataory Drugs (NSAIDS) kamaibuprofen, naproxen na kadhalika.


7.Hakikisha vifaa sahihi ndivyo vilivyotumiwa- Hakikisha ya kwamba  vifaa vinavyotumiwa ni vile ambavyo havina   madini ya Nickel, pini zenye ubora na vipachiko vya aina mbalimbali ambavyo ni vya ubora wa hali ya juu. Pini na vipachiko vidogo vinaweza kutoka na kusogea kutoka katika sehemu vilipopachikwa na hivyo kukuletea madhara makubwa.

8.Mfumo wa maisha- Kipachiko cha katika maeneo ya tumboni (kitovuni, chini ya kitovu nk) huvutia kwa mwanamke wenye umri mdogo wa miaka ya ishirini na huleta picha mbaya kwa wanawake wale waliofikia umri wa miaka thelathini na kuendela. Unatakiwa uangalie  na aina ya taaluma yako  kama inaendana na vitu vya aina hivi, mathalani wewe ni mwanamume unafanya kazi ya mhudumu wa afya, mwalimu, askari,  unafanya kazi kwenye ofisi, muuzaji bidhaa kwa wateja, mtoa huduma za kijamii, halafu unavaa herini kwenye masikio, ha! Watu watakuchukuliaje?Hakuna atakaye kuelewa au kukubali kuhudumiwa na wewe. Pia angalia kama  mila, desturi, dini  yako kama inakubali mambo haya kwani itakuwa jambo la aibu sana kama utatoga mwili wako  bila kuzingatia mazingira unayoishi kwani binadamu tunaishi kulingana na mazingira yetu. Hii sio kwa wanaume tu hata kwa wanawake, kabla ya kutoboa/kuchora  sehemu husika zingatia  taaluma yako, mila, desturi,mazingira,  dini yako nk.

9.Fuata maelekezo vizuri- Fuata maelekezo unayopewa vizuri jinsi ya kujikinga na maambukizi baada ya kutoboa/kuchorwa mwili wako, namna ya kusafisha sehemu husika nk.
 10.Fahamu madhara ya kutoboa/kuchorwa sehemu husika- Fahamu kuhusu madhara ya kutoboa/kuchorwa sehemu husika kwanza kabla ya kutoboa/kuchorwa ili uweze kujiepusha na madhara hayo.Pia unatakiwa ujue sehemu hiyo unayotoboa/kuchora, kidonda chake kinapona baada ya muda gani na maumivu yake huchukua siku ngapi kuisha? Hatma ya afya yako ipo mikononi mwako!

Chanzo cha mwanamke kukosa hedhi (amenorrhea)

00:08 Add Comment
Tatizo la kukosa hedhi ni jambo ambalo linawakumba wanawake wengi waliovunja ungo. Aidha suala hili limekuwa likiwaletea usumbufu mwingi wa kisaikolojia wanawake wengi waliowahi kukumbana nalo.

Tatizo la kukosa hedhi au amenorrhea linaweza kutokea awali kabisa (primary) au baadaye kabisa maishani (secondary).

Primary amenorrhea ni hali ya kukosa hedhi inayoweza kumtokea msichana aliye katika umri wa kuvunja ungo na ambayo huweza kuendana na hali ya kukosa mabadiliko ya kubalehe kama vile kuota matiti au nywele za kinena; au msichana anaweza kuwa na mabadiliko ya kubalehe lakini asipate hedhi.

Secondary amenorrhea ni hali ya kukosa hedhi inayomtokea mwanamke ambaye si mjamzito, hanyonyeshi, na ambaye hajavuka umri wa kukosa hedhi (menopause) na wala hatumii njia za uzazi wa mpango kama vile sindano au vidonge, na ambaye hapo awali alikuwa akipata hedhi kama kawaida lakini akasimama kwa miezi mitatu au zaidi.
Mwanamke hupataje hedhi?

Ili mwanamke aweze kuwa na mzunguko ulio sahihi wa hedhi, ni lazima matezi yake ya hypothalamus napituitary pamoja na kiwanda cha kutengeneza mayai ya kike (ovaries) na mji wa mimba (uterus) vifanye kazi zake sawasawa.

Hypothalamus huchochea tezi la pituitary kuzalisha hormone chochezi ya follicle au follicle-stimulating hormone (FSH) pamoja na homoni ya luteinizing (LH). Hizi FSH na LH kwa pamoja huchochea ovarieskuzalisha homoni za estrogen pamoja na progesterone. Kazi za estrogen na progesterone ni kusababisha mabadiliko katika ukuta wa uterus yaani endometrium ikiwepo kupata hedhi. Ili damu ya hedhi iweze kutoka nje, njia ya uzazi ya mwanamke haina budi kuwa huru yaani isiyo na matatizo yeyote yale.

Amenorrhea husababishwa na nini?
Visababishi vya amenorrhea vyaweza kugawanywa katika makundi makuu matatu, vile vinavyohusisha matatizo katika mfumo wa homoni, vile vinavyohusisha matatizo ya kimaumbile katika njia ya uzazi ya mwanamke na vile vinavyohusisha mabadiliko katika mwili wa mwanamke.

1.       Matatizo katika mfumo wa homoni: Matatizo katika mfumo wa homoni yanaweza kuwa katika tezi za hypothalamus, pituitary au ovary.

1.       Matatizo katika Hypothalamus: Matatizo katika hypothalamus yanayoweza kusababisha mwanamke kukosa hedhi ni pamoja na
§  Uvimbe katika ubongo karibu na tezi ya pituitary
§  Ukosefu au upungufu wa homoni zinazochochea kukua na kufanya kazi kwa via vya uzazi. Ugonjwa huu hujulikana kama Kallmann syndrome
§  Lishe duni na utapia mlo
§  Uzito mdogo kuliko kawaida (kukonda kwa kupitiliza)

2.       Matatizo katika tezi ya Pituitary: Vyanzo vinavyohusisha tezi ya pituitary ni pamoja na
§  Kuwepo kwa kiwango kikubwa cha homoni ya prolactin katika damu au kwa kitaalamuProlactinemia. Prolactin ni homoni inayochochea uzalishaji wa maziwa wakati wa kunyonyesha. Hali ya kuwa na prolactin nyingi katika damu inaweza kutokea iwapo kuna uvimbe unaoitwa (prolactinoma) katika tezi ya pituitary.
§  Kuwepo kwa uvimbe mwingine wowote katika tezi ya pituitary.
§  Pituitary kushindwa kufanya kazi baada ya seli zake kufa, hususani iwapo mama alipoteza damu nyingi wakati wa kujifungua.
§  Kuharibika kwa tezi ya pituitary baada ya seli zake kushambuliwa na mfumo wa kinga ya mwili.
§  Kuwa na historia ya kupata tiba ya mionzi inayohusisha tezi ya pituitary.

3.       Matatizo katika ovary: Vyanzo vinavyohusisha matatizo katika viwanda vya kuzalisha mayai ya kike yaani ovaries ni pamoja na
§  Kutozalishwa kabisa kwa mayai (Anovulation)
§  Kuwepo kwa kiwango kingi cha homoni za kiume katika damu (Hyperandrogenemia)
§  Ovary kuwa na vifukovifuko (Polycystic ovarian syndrome) na kushindwa kufanya kazi zake vizuri. Haya ni matatizo ya homoni ambayo huwapata baadhi ya wanawake walio katika umri wa kuzaa
§  Kufa na kushindwa kufanya kazi kwa ovary kabla ya muda wake
§  Ugonjwa wa kuzaliwa unaoitwa Turner syndrome ambao humbatana na kukosekana kwa ovary au ovary kuwa changa kuliko kawaida, msichana kushindwa kuvunja ungo na msichana kuwa na kimo kifupi kuliko kawaida. Ugonjwa huu hutokana na matatizo ya kijenitikia (genetic disease)
§  Ukosefu wa kimaumbile wa ovary ambao hutokea wakati wa ukuaji
§  Kufa kwa ovary baada ya seli zake kushambuliwa na mfumo wa kinga ya mwili
§  Historia ya kuwahi kupata tiba ya mionzi au madawa yanaathiri ovary
§  Ugonjwa wa kurithi wa Galactosemia unaoambatana na kuwa na kiwango cha juu cha sukari aina ya galactose katika damu

2.       Matatizo ya kimaumbile katika njia ya uzazi: Matatizo ya kimaumbile katika njia ya mfumo wa uzazi wa mwanamke yanayoweza kusababisha ukosefu wa hedhi ni pamoja na

1.       Mwanamke/msichana kuzaliwa bila kuwa na uke, shingo ya uzazi au mji wa mimba (uterus)

2.       Kuta za uterus zinazotazamana kujishikiza pamoja

3.       Utando unaozunguka uke (hymen) kuziba kabisa na kukosekana kwa tundu la kupitishia damu ya hedhi (imperforate hymen)

4.       Kuwepo kwa utando unaokatiza katika uke unaozuia damu ya hedhi kushindwa kutoka

3.       Mabadiliko katika mwili wa mwanamke: Mambo yanayoweza kuathiri mwili wa mwanamke na kumfanya ashindwe kupata hedhi ni pamoja na

1.       Kula kiasi kidogo sana cha chakula kuliko kawaida au kula kupita kiasi
2.       Unene uliopitiliza au kupungua uzito/kukonda isivyo kawaida
3.       Uwepo wa magonjwa sugu kama kifua kikuu
4.       Utapiamlo
5.       Msongo wa mawazo
6.       Matumizi ya madawa ya kulevya
7.       Matumizi ya baadhi ya madawa hususani baadhi ya dawa za kutibu magonjwa ya akili
8.       Kuwa na hofu iliyopitiliza
9.       Kufanya mazoezi ya mwili kupita kiasi

Dalili za Amenorrhea ni zipi?
Kukosa hedhi siyo ugonjwa bali ni dalili ya kuwepo kwa tatizo au ugonjwa fulani katika mwili. Kulingana na ugonjwa unaosababisha tatizo hili, kukosa hedhi kunaweza kuambatana pia na
·         Matiti kutoa maziwa wakati mwanamke si mjamzito na wala hanyonyeshi, maumivu ya kichwa na matatizo katika kuona vitu ambavyo kwa pamoja vinaweza kuashiria uwepo wa uvimbe katika ubongo
·         Mwanamke kuwa na nywele na vinyweleo vingi mwilini na kuota ndevu kama mwanaume hali inayoashiria kuwepo kwa wingi kwa homoni za kiume za androgen
·         Ukavu katika uke, kutoka jasho sana wakati wa usiku, au mabadiliko katika kupata usingizi vinaweza kuashiria matatizo katika ovary
·         Kuongezeka uzito kupita kiasi au kupungua kwa uzito isivyo kawaida
·         Mwanamke kuwa na mhemko kuliko kawaida yaweza kuashiria kuwepo kwa matatizo ya kiakili na kisaikolojia

Uchunguzi na vipimo
Msichana yeyote aliyefikia umri wa kubalehe na kuvunja ungo na ambaye bado hajaanza kupata mabadiliko yeyote ya kubalehe katika mwili wake hana budi kumuona daktari kwa ajili ya uchunguzi zaidi. Aidha msichana aliyefikia umri wa miaka 16 na ambaye bado hajaanza kupata hedhi anatakiwa pia kumuona daktari kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Kwa wanawake waliokuwa wakipata hedhi kama kawaida lakini ghafla wakaacha kupata kwa muda wa miezi mitatu mfululizo au zaidi nao pia hawana budi kumuona daktari kwa ajili ya uchunguzi wa tatizo hili.
Vipimo vifuatavyo vinaweza kufanywa kuchunguza sababu za kukosa hedhi kwa mwanamke:
·         Kupima damu kwa ajili ya kuchunguza kiwango cha homoni za FSH, LH, TSH na prolactin ambazo uzalishwaji wake unachochewa na tezi ya pituitary, na pia kupima kiwango cha homoni ya estrogen inayozalishwa na ovary.
·         Kipimo cha ultrasound ya nyonga kwa ajili ya kuchunguza uwepo wa matatizo katika njia ya uzazi na pia kuchunguza hali ya ovary.
·         CT scan au MRI ya kichwa kwa ajili ya kuchunguza uwepo wa matatizo kwenye tezi ya pituitary au hypothalamus.
·         Vipimo vya kufahamu ufanyaji kazi wa tezi ya thyroid
·         Kupima damu ili kufahamu kiwango cha homoni ya prolactin katika damu
·         Kuchunguza uterus kwa kutumia aina ya X-ray inayoitwa Hysterosalpingogram na kipimo kingine kiitwacho Hysteroscopy ambacho huchunguza chumba cha uterus.

Matibabu ya kukosa hedhi
Matibabu ya kukosa hedhi yanaweza kufanyika nyumbani bila kuhitaji dawa, ingawa pia, kutegemeana na chanzo cha tatizo, yanaweza kuhitaji dawa na hata upasuaji wakati mwingine.

1.       Matibabu yasiyohitaji dawa
o    Baadhi ya wanawake wanaopata tatizo la kukosa hedhi kwa sababu ya kujinyima kula (wanaofanya dieting) na hivyo kupata upungufu wa virutubisho mwilini, wanashauriwa kula lishe bora.
o    Baadhi ya wanawake wanaopata tatizo hili la kukosa hedhi kwa sababu ya kuongezeka uzito kupitiliza, wanashauriwa kuwa makini katika aina ya vyakula wanavyokula ili kuwa na uzito unaotakiwa.
o    Wanawake wanaokosa hedhi kwa sababu ya kufanya mazoezi ya mwili kupita kiasi wanashauriwa kujiwekea kiasi katika ufanyaji wao wa mazoezi.
o    Iwapo kukosa hedhi kumesababishwa na msongo wa mawazo, ni jambo jema kutafuta njia za kushughulikia matatizo hayo na kuyatatua ili kuondoa msongo wa mawazo
o    Inashauriwa kutokuvuta sigara na kuacha kunywa kunywa pombe.

2.       Matibabu yanayohitaji dawa: Matibabu ya kukosa hedhi hutegemea chanzo cha tatizo. Matibabu huelekezwa katika kutibu chanzo, na iwapo chanzo cha tatizo ni matatizo ya kimaumbile, upasuaji unaweza kufanyika. Kwa wanawake wenye matatizo ya kuwa na kiwango kingi cha prolactin, daktari anaweza kushauri matumizi ya dawa aina ya bromocriptine au pergolide. Kwa wanawake wenye upungufu wa homoni ya estrogen au wale wenye matatizo katika ovary zao, dawa zenye kurejesha homoni hiyo zaweza pia kutumika. Wakati mwingine dawa za uzazi wa mpango zaweza kutumika kurejesha mzunguko wa hedhi na pia kusaidia kuongeza kiwango cha homoni ya estrogen mwilini.

3.       Upasuaji: Upasuaji unaweza kufanywa iwapo kuna
o    Uvimbe katika ubongo unaoathiri tezi ya pituitary na hypothalamus
o    Matatizo katika njia ya uzazi ya mwanamke

Je kukosa hedhi kunaweza kusababisha nisipate mtoto?
Ikumbukwe kuwa, kukosa hedhi si ugonjwa bali ni dalili ya kuwepo tatizo hivyo basi iwapo tatizo hilo lina uhusiano na kutunga mimba na kupata mtoto, uwezekano wa kupata mtoto utakuwa mdogo ikiwa tatizo hilo halitashughulikiwa. Matatizo kwenye tezi za pituitary, hypothalamus pamoja na ovary ambayo yana uhusiano mkubwa na kukosa hedhi, husababisha pia tatizo la ugumba. Iwapo matatizo hayo yatashughulikiwa ipasavyo, uwezekano wa kupata kupata hedhi na hatimaye kupata mimba huwa mkubwa.

Maana Ya Magonjwa Nyemelezi Kwa Binadamu

15:59 Add Comment
Magonjwa nyemelezi ni yale ambayo hushambulia mwili wa binadamu pale uwezo wa kinga ya mwili kupigana na vimelea vya magonjwa unaposhuka.
Ni magonjwa ambayo katika hali ya kawaida hayategemewi kujitokeza kwa mtu mwenye kinga kamili ya mwili.
Kwa kawaida mwili wa binadamu yeyote umeumbwa na kinga ya mwili ya asili ambayo lengo lake kuu ni kuulinda mwili dhidi ya vimelea vya magonjwa.Inapotokea kimelea (vimelea) kuingia katika mwili wa binadamu kwa njia yoyote (kunywa au kula vimelea,kugusana na majimaji au ngozi ya mtu mwenye vimelea,au kupitia damu yenye vimelea n.k), mwili hutengeneza kingamwili (antibodies) ambazo hupigana na vimelea hivyo ili kuuweka mwili katika afya njema kama hapo awali.

Kushuka kwa kinga ya mwili hupelekea mwili kushindwa kupigana na vimelea vya magonjwa hivyo kusababisha kushambuliwa na magonjwa.Ifahamike kwamba baadhi ya vijidudu(microorganisms) pia hupatikana katika mwili wa binadamu bila madhara yoyote (normal flora) kama vile kwenye ngozi, mfumo wa chakula, ukeni, uumeni n.k Hata hivyo vijidudu hivi huweza kuwa chanzo cha magonjwa iwapo kinga ya mwili itashuka.
`

Vitu gani hupelekea kushuka kwa kinga ya mwili?

Sababu mojawapo kubwa ya kushuka kwa kinga ya mwili haswa katika nchi zilizopo chini ya jangwa la Sahara ni Ukimwi/VVU.Hata hivyo ieleweke kwmba si kila mtu mwenye upungufu wa kinga mwilini ana VVU.

Kuna sababu nyingine nyingi ambazo husababisha kwa njia moja au nyingine kushuka kwa kinga ya mwili.Zifuatazo ni baadhi tu ya sababu hizo;

Utapiamlo, Kuugua mara kwa mara,Sababu za kijenetiki (kurithi),Madhara kwenye ngozi,Msongo wa mawazo na Ujauzito. Madawa ya Kutibu saratani, Matumizi ya muda mrefu ya antibayotiki (antibiotics),steroidi (steroids) na madawa ya kushusha kinga mwilini (immunosuppressant drugs)) ambayo hutumika wakati wa kupandikiza viungo mwilini kama figo n.k

Magonjwa nyemelezi husababishwa na vijidudu mbalimbali kama bacteria,virusi,fangasi na bakteria.

Bakteria

Baadhi ya magonjwa yasababishwayo na bakteria ni kama yafuatayo;

Kifua Kikuu (TB)
Ugonjwa huu husababishwa na kimelea kiitwacho Mycobacterium tuberculosis ambacho ni moja katika kundi la Mycobacterium Avium Complex (MAC).Kushuka kwa kinga ya mwili hupelekea kulipuka kwa vimelea vya kifua kikuu ambavyo hupatikana, pamoja na viungo vingine, zaidi kwenye mapafu.
Dalili za kifua kikuu ni pamoja na kikohozi na homa (haswa nyakati za usiku) kwa zaidi ya wiki mbili.Kutokwa jasho usiku (mara nyingi jasho huwa jingi mpaka kulowesha shuka),kupungua uzito (zaidi ya kilo moja na nusu ndani ya mwezi), Kichomi na kukohoa damu.
Ugonjwa huu pia huweza kupelekea kupata homa ya uti wa mgongo(meningitis) ambayo huambata na dalili kama kuumwa kichwa, kichefu chefu na kutapika ikifutiwa na kuongezeka kwa joto la mwili na maumivu na kukaza kwa shingo.

Nimonia (Pneumonia)
Huu ni ugonjwa ambao kwa kiasi kikubwa huathiri mfumo wa hewa na haswa mapafu.Baadhi ya vimelea viletavyo nimonia ni kama Pneumococcus ,Haemopilus influenza, Mycoplasma (haswa kwa watoto) pia Klebsiella, Staphylococcus aureus, Pseudomonas aeuroginosa (kwa wagonjwa waliolazwa mahospitalini) na wengineo.
Ugonjwa huu huanza ghafla na dalili zake ni kama homa kali, kikohozi, maumivu wakati wa kupumua, baridi na kutetemeka.

Ugonjwa wa Ngozi
Huu husababishwa na vimelea vya Staphylococcus aureus.Vimelea hivi huishi katika mwili wa binadamu (kwenye ngozi ya kichwa na kinena (groins) na kwapani) bila madhara.Pia hupatikana kooni na katika utumbo mpana na mkojo.
Vimelea vya Staphylococcus husambaa kwenda sehemu nyingine ya mwili kutoka kwenye usaha, mgusano na ngozi ya mwenye maradhi, kutumia taulo, matandiko,vifaa vya mtu aliyeathirika n.k

Dalili zake ni pamoja na chunusi, majipu, kubabuka kwa ngozi na magamba magamba katika ngozi.


Magonjwa ya Virusi


Magonjwa yasababishwayo na virusi ni kama;

Ugonjwa wa Malengelenge
Husababishwa na virusi vya Herpes Simplex.Hivi vimegawanyika katika Herpes Simplex Virus-1 (HSV-1) na Herpes Simplex-2 (HSV-2).Virusi vya HSV-1 vyaweza ambukizwa kupitia ngozi laini (mucous membranes) za mwili na kubusiana.Huweza kusababisha mwasho kwenye midomo,ulimi,fizi za meno au kingo za juu za kinywa (buccal mucosa).Kwa upande wa virusi vya HSV-2 hivi huweza kusababisha michubuko na maumivu kwenye uume,uke na njia ya haja kubwa.

Katika kiwango cha juu cha ugonjwa viungo vingine vya mwili kama macho, njia ya chakula, mfumo wa fahamu na na njia za mfumo wa hewa huathirika.

Dalli balimbali za ugonjwa huu ni malengelenge (blisters), mwasho na muunguzo.Kushindwa kumeza au kupata maumivu wakati wa kumeza (haswa chakula),tezi kuvimba na maumivu wakati wa haja kubwa au ndogo.

Mkanda wa jeshi
Husababishwa na kirusi kiitwacho Varicella Zoster (VSV).Mara nyingi hutokana na kuamshwa kwa ugonjwa ambao ulikuwepo mwilini hapo Awali (reactivation of an earlier infection).Mbali ya kuathiri ‘uwanda’ (dermatome) moja au zaidi wa mishipa ya fahamu (neva),pia huweza kudhuru jicho (herpes zoster opthalmicus) na sikio (herpes zoster oticus).
Dalili zake ni maumivu makali katika ‘uwanda’ ulioathirika, homa, vipele, maumivu ya kichwa, uchovu na maumivu ya macho kutokana na mwanga (photophobia).

Maumivu ya Retina
Kwa lugha ya kitaalamu huitwa CMV Retinitis na husababishwa na kirusi kiitwacho Cytomegalovirus (CMV).Kirusi hiki, mbali ya kuathiri jicho na haswa retina, pia huathiri viungo vingine kama mapafu na kusababisha nimonia, utumbo mpana na mfumo wa fahamu ambako husababisha maumivu.

Dalili zake ni pamoja na kutoona vizuri, macho kuuma, kutokwa na machozi kwa wingi.Kutopata matibabu mapema huweza kusababisha upofu.Pia Huweza kuathiri viungo vingine na kusababiosha homa, nimonia, kichefuchefu, kuharisha na kupungua uzito.

Magonjwa yatokanayo na Fangasi

Fangasi pia huweza kujitokeza iwapo kinga ya mwili itashuka.

Kandidiasisi
Ugonjwa huu uliozoeleka pia hujulikana kwa kitaalamu kama Candidiasis.Kandidiasisi husababishwa na fangasi aitwaye Candida albicans ambaye huathiri kinywa, mfumo wa chakula,uke na mfumo wa hewa.Kandidiasisi katika uke huweza tokea kwa mwanamke mwenye afya asiye na VVU.

Dalili za Kandidiasisi katika kinywa ni pamoja na kubadilika kwa ladha,maumivu kwenye ulimi,utando mweupe kwenye ulimi na kingo za juu za kinywa (buccal mucosa),kushindwa kumeza,maumivu wakati wa kumeza chakula ikiwa fangasi imesambaa sana. Pia mwasho na maumivu ukeni pamoja na kutokwa na majimaji meupe ukeni.

Homa ya Uti wa mgongo
Homa ya utiw amgongo au Meningitis kwa kitaalamu husababishwa na fangasi aitwaye Cryptococcal neoformans.Uti wa mgongo utokanao na aina hii ya fangasi huweza kusababisha kifo usipotibiwa.Aina hii ya fangasi ambayo huathiri zaidi ubongo na uti wa mgongo, hutokana na kuvuta hewa yenye vumbi litokanalo na ndege lenye vimelea vya ugonjwa.
Baadhi ya dalili zake ni homa, kutoona vizuri,macho kuuma kutokana na mwanga,kuchanganyikiwa akili,maumivu ya kichwa ka kukakamaa na kuuma kwa shingo.

Histoplasmosisi
Aina hi ya fangasi hutokana na vimelea vya Histoplasma capsulatum.Fangasi huyu huathiri mapafu pamoja na viungo vingine.Dalili zake ni homa,uchovu,kupungua uzito na kupumua kwa shida.Pia kukohoa na kuvimba kwa tezi kwaweza kutokea.


Nimonia

Kama bakteria na fangasi pia huweza kusababisha nimonia ijulikanayo kwa kitaalamu kama Pneoumocystis Pneumonia (PCP).Vimelea vya Pneumocystis jiroveci (awali vilijulikana kama Pneuomocystis carinii) huathiri mfumo wa hewa.Fangasi huyu pia huweza kuathiri viungo vingine kama ini,wengu (spleen) na figo katika baadhi ya wagonjwa.
Dalili zake ni kikohozi kikavu,kifua kubana,kupumua kwa shida,homa,kuishiwa pumzi na kutokwa jasho nyakati za usiku.

Magonjwa yatokanayo na Protozoa

Toksoplasmosisi ya Ubongo
Cerebral toxoplasmosis, kama ujulikanavyo kitaalamu,hutokana na kuamshwa kwa ugonjwa wa awali kutokana na vimelea vya Toxoplasma gondii (kimelea kiwezacho kuishi ndani ya seli kinachoathiri ndege,wanyama na binadamu).Kimelea hiki kiathiricho zaidi mfumo wa fahamu,hupatikana kwenye nyama isiyopikwa vizuri na mavi ya paka.Huathiri zaidi ubongo na kusababisha maumivu ya kichwa,kuchanganyikiwa,udhaifu wa viungo,homa,kupoteza fahamu,kupooza na kifafa.

Kriptosporidiosisi
Huu ni ugonjwa utokanao na vimelea vya Cryptosporidium.Huathiri zaidi mfumo wa chakula na hutokana na kutumia kwa maji au chakula vilivyoathirika na vimelea vya ugonjwa huu.Dalili zake ni kuharisha sana kiasi cha kusababisha kupungukiwa na maji mwilini (dehydration),maumivu wakati wa haja kubwa, kichefuchefu na kutapika.Wagonjwa wa aina hii huwa na joto la mwili la kawaida.

Matibabu na Ushauri

Aina ya matibabu hutegemea na aina ya ugonjwa na mtu, pia kutokana na kuwepo kwa Ukimwi/VVU hutegemea kiwango cha seli za CD4 mwilini.Iwapo una dalili kati ya zilizotajwa hapo juu ni vyema kumona daktari kwa uchunguzi zaidi.
Ni vyema kuzingatia kuwepo kwa dalili zilizotajwa hapo juu hakumanishi kuwa muathirika ana VVU na si kila mwenye VVU huwa na dalili hizo.Pia kujitokeza kwa dalili kunaweza kutofautiana kati ya mtu na mtu.Hata hivyo ni vyema kupima afya yako kila mara haswa VVU ili kujua chanzo cha kupungua kwa Kinga ya mwili ambayo huweza kupelekea kupata magonjwa nyemelezi

Mambo Muhimu Unapotaka Kushika Ujauzito

15:38 Add Comment
Habari wasomaji, hapa nilitaka tuwezze kuelekezana mambo yakuzingatia na kufata iwapo unahitaji kushika mimba au unataka kusababisha mimba.

Si tu kujua siku za Ovulation ni lini basi sio kigezo cha mimba kuweza kutungwa ila pia kuna mambo kadhaa ya kufanya na kufatwa ili lengo la mimba liweze kutimia.

Kuna sababu mbalimbali zinazoweza kumfanya mtu asishike mimba. Sababu hizo zinaweza zikawa zinamhusu mwanamke, mwanamume au wakati mwingine kutojulikana kabisa hali hiyo imesababishwa na nini.

Wataalamu wanasema kwamba kwa miaka 20 iliyopita matatizo yanayohusu kushindwa kuzaa yameongezeka kwa kiwango kikubwa na asilimia 25 ya watu wanaotaka kubeba mimba na kuzaa mtoto wanakabiliwa na tatizo hilo.

Ni kweli kuwa kwa kawaida watu wengi hubeba mimba na kujaaliwa mtoto pale tu wanapofanya tendo la ndoa. Lakini jambo hilo halitokei kwa watu wote na ingawa kwa baadhi ya watu kila kitu huonekana kwenda sawa lakini pia hushindwa kubeba mimba.
Utafiti unaonyesha kwamba katika kila familia au 'couples' 5 zinazojamiiana katika wakati muafaka wa ovulation ni moja tu ndio hufanikiwa kupata mtoto, huku karibu wanawake 9 kati ya 10 wakifanikiwa kushika mimba baada ya kujaribu kutafuta mtoto kwa mwaka mmoja mzima bila kuzuia mimba.

Hivyo basi nawaomba wale ambao wamekuwa wakifanya jitihada za kufuata maelekezo ili waweze kushika mimba lakini hawakufanikiwa, wasife moyo kwani ipo siku jitihada zao hizo zitazaa matunda.

Mambo ya kuzingatia iwapo unataka kushika mimba…
  • Kwanza kabisa ni kuhakikisha kuwa kabla ya yote unaonana na dokta wako au unakwenda hospitalini na kufanyiwa vipimo ili kujua kama afya yako iko salama au la kwa ajili ya kushika mimba. Baadhi ya vipimo vinavyoshauriwa kufanywa ni pamoja na
1. General examination au uchunguzi wa jumla.

2. Kipimo cha kensa au Pap smear.

3. Kipimo cha magonjwa ya zinaa (STD) kama vile Chlamydia ambao wanaweza kuathiri uwezo wako wa kushika mimba.

4. Kipimo cha damu cha kuangalia kama una upungufu wa damu, Rh na kinga yako ya mwili dhidi ya ugonjwa wa Rubella.

5. Kipimo cha mkojo cha kuchunguza iwapo una ugonjwa wa kisukari. Ugonjwa wa kisukari huweza kumzuia mtu asishike mimba hata iwapo mzunguko wake wa mwezi uko sawa, anapata Ovulation na kidhahiri anaonekana hana tatizo lolote.

6. Kama una paka nyumbani au unakula sana nyuma (red meat) pengine si vibaya pia kupima kipimo cha Toxopmasmosis infection.

7. Kuyajua na kuzingatia baadhi ya mambo yanayoathiri kushika mimba ambayo ni pamoja na:
  • Ingawa unene unaweza kumzuia mtu asishike mimba lakini kufanya mazoezi sana na kuwa na uzito mdogo sana wa zaidi ya kilo 50 huweza pia kumsababisha mtu asishike mimba. Mazoezi ya kupindukia pia huathiri homoni mwiilini
  • Kuwa na fikra nyingi na msongo wa mawazo 'stress' huweza pia kauthairi uwezo wa mtu wa kushika mimba.
  • Kutokula vizuri na kutopenda kula kwani humkosesha mwanamke au hata mwanamme baadhi ya virutubisho muhimu vinavyotakiwa kwa ajili ya kufanikisha suala la kushika mimba (nitazungumzia vyakula vinavyosaidia kushika mimba baadaye)
  • Sigara, marijuana na pombe ni miongoni mwa vitu ambavyo vinaweza kuathiri uwezo wa kubeba mimba. Mwanamke anayetaka kubeba mimba anashauriwa aache kunywa pombe na kuvuta sigara. Mwanamume pia anashauriwa kuacha kuvuta sigara kwani sigara huathiri kiwango cha mbegu za kiume za mwanamme.

Yafuatayo ni baadhi ya mambo yanayomsaidia mwanamke kushika mimba:
  • Anza kutumia vidonge vya Folic Acid, vidonge hivyo mbali ya faida nyinginezo humkinga mtoto atakayezaliwa na magonjwa ya ubongo. (Neural Tube Defect) kama vile Spinal Bifida na mengineyo. Dozi ni kwa uchache miligramu 0.4 za Folic acid kwa siku, miezi mitatu kabla ya kuanza hata kutafuta mtoto.
  • Endelea tu na tendo la ndoa bila kuchoka au kukata tamaa, lakini ni bora nguvu zihifadhiwe kwa siku chache kabla ya Ovulation na siku kadhaa baada ya hapo ili mwanamume aweze kuboreshe na kuhifadhi mbegu zake kwa ajili ya siku hizo, Usikimbie chooni au bafuni baada tu ya kukutana kimwili na mwenzio. Kulala kwa dakika kadhaa baada ya tendo la ndoa huongeza uwezo wa mbegu ya kiume kuweza kuendelea kukutana na yai la kike na hivyo kuongeza uwezekano wa kubeba mimba.
  • Jiepushe kunywa kahawa na vinywaji vinginevyo vyenye caffeine. Waataalamu wanasema caffeine huweza kukuongezea matatizo ya kushindwa kushika mimba.
  • Jiepushe na kutumia dawa za aina yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinazonunulika maduka ya dawa bila ulazima wa cheti cha daktari au Over-the-counter drugs inabidi zitumiwe baada ya kushauriana na daktari.
  • Usitumie baadhi ya vitu vinavyoufanya uke uwe na hali itakayoua mbegu za kiume au kupunguza majimaji yake. Vitu hivi ni kama spray mbalimbali na tampons zinazotumiwa na wanawake ili kuufanya uke uwe na harufu nzuri. Mafuta ya aina mbalimbali na jeli kwa ajili ya kulainisha sehemu za siri, mafuta ya kula (vegetable oils) glycerin na mate. Vitu kama hivi kufanya Ph ya uke isiwe ya kawaida na huweza kuua mbegu ya kiume, kusababisha baadhi ya magonjwa ya wanawake au kupunguza majimaji ya ukeni ambayo yanatakiwa ili kusafirisha mbegu za kiume.
  • Hakisha mwenzi wako hafanyi kazi au hawi katika mazingira yenye mada hatari ambazo hupunguza uwezo wa mbegu za kiume au kutungwa mimba. Kufanya kazi kwenye mazingira ya joto kali sana kama vile mwanaume wanaofanya kazi kwenye matanuri ya kupika mikate, viwanda vya mafuta na miale hatari baadhi ya wakati huwa na matatizo ya kutozaa. Hivyo kabla mwanamke hajaanza kujilaumu kwa nini hashiki mimba, mwanamme wake pia anapaswa kufanyiwa uchunguzi kamili kuhusiana na suala hilo. Pengine ni suala ambalo wengi hatulijui kwamba katika tiba iwapo mke na mume au mtu na mwenzi wake wana tatizo la kutopata mtoto, wawili hao kwa pamoja hupaswa hufanyiwa vipimo na wala sio mwanamke mwenyewe. Hivyo iwapo unashindwa kushika mimba, hakikisha pia mwenzi wako hana tatizo pia.

Wanaume pia kama walivyo wanawake hukabiliwa na matatizo mengi tu yanayosababisha familia kukosa watoto. Matatizo kama vile upungufu wa mbegu za kiume, uchache wa mbegu, kutokuwa na kasi mbegu na mengineyo ni miongoni mwa matatizo kibao ambayo mwanamume anaweza kuwa nayo na kukosa mtoto. Hivyo tabia ya kuwatizama wanawake kwa jicho la lawama katika jamii na kuwanyooshe kidole pale mimba inaposhindikana kushika ni kinyume cha ukweli wa kitiba na uhalisia.
  •  Usichoke kufuata mzunguko wako wa Ovulation na kufanya tendo la ndoa katika wakati ambao mwili wako (ewe mwamamke) uko katika siku za kuweza kushika mimba.

Tatizo La Ugumba Kwa Binadamu

08:36 Add Comment
Ugumba ni hali inayotokea iwapo watu wawili, mwanaume na mwanamke wanapokutana kimwili (au kujamiana) bila kutumia njia yoyote ile ya upangaji uzazi kwa muda wa miezi 12 na kutoweza kushika mimba au kupata ujauzito.

Kuna aina mbili za ugumba;
Ugumba wa asili (Primary infertility) - Hii ni pale ambapo mwanaume na mwanamke hawajawahi kutunguisha mimba kabisa maishani mwao hata baada ya kujamiana au kukutana kimwili kwa muda wa mwaka mmoja bila kutumia njia yoyote ile ya kuzuia kupata mimba.

Ugumba unaotokea baadaye maishani (Secondary infertility) - Hii ni pale ambapo wote wawili, mwanamke na mwanaume wameshawahi kupata ujauzito au kutungisha mimba angalau mara moja maishani mwao na baada ya hapo hawajafanikiwa kupata au kutungisha mimba tena.
Asilimia 30-40 ya tatizo la ugumba huwakumba wanaume na asilimia 40-50 ya tatizo hili huwakumba wanawake, wakati asilimia 10-30 zilizobakia ya tatizo hili husababishwa kwa pamoja na matatizo kati ya wanaume na wanawake, hapa sababu halisi hazijulikani.
Kwa wale wenye afya njema, uwezekano wa kupata au kutungisha mimba iwapo watajamiana mara kwa mara kwa mwezi ni asilimia 25-30. Wanawake hufikia kilele cha kupata ujauzito (peak fertility) wakiwa kwenye miaka ya ishirini. Mwanamke aliye na umri wa zaidi ya miaka 35 (au baada ya miaka 40) ana uwezekano wa kupata ujauzito kwa asilimia 10.

Je mimba hutungwa vipi?
Mimba hutungwa baada ya mwanamke kutoa yai kutoka katika moja ya viwanda vyake vya mayai ya kike yaani ovaries,kitendo hiki hujulikana kama ovulation. Yai husafiri hadi kwenye mfuko wa uzazi ujulikanao kama uterus (womb) kupitia kwenye mirija ya uzazi inayojulikana kama mirija ya fallopian.
Mbegu moja ya kiume (sperm) ni lazima itungishe au iungane (fertilize) na yai au mayai ya kike (ovum au ova) wakati yai likielekea kwenye uterus. Baada ya mbegu ya kiume na yai la kike kuungana, muunganiko uliotengenezwa yaani kiinitete (embryo) hushuka mpaka kwenye mfuko wa uzazi na kujiwekeza hapo ili kiendelee kuwa kiumbe.
Tatizo la ugumba linaweza likawa ni la nwanaume au mwanamke pekee ingawa wakati mwingine wote wawili wanaweza kuwa na tatizo hili.


Ni sababu zipi zinazoleta tatizo la ugumba (infertility) ?
Kwa wanawake ;
Tatizo la ugumba linaweza kutokea wakati wa;

  • Yai au kiumbe kilicho ndani ya mfuko (uterus) wa uzazi kushindwa kukua hadi kufikia kuwa mtoto.
  • Mayai yaliyo ndani ya mfuko wa uzazi kushindwa kujishikiza kwenye ukuta wa mfuko wa uzazi (uterus lining)
  • Matatizo kwenye njia ya kupita yai au mayai wakati yanakwenda kwenye mfuko wa uzazi (uterus).
  • Matatizo ya mayai ya uzazi (ovaries) kushindwa kutoa mayai (eggs).
  • Tatizo la ugumba kwa wanawake husababishwa na;
  • Matatizo ya autoimmune disorders kama antiphospholipid syndrome (APS)
  • Matatizo katika uterus na shingo ya kizazi (cervix) kama uvimbe (fibroids or myomas) na birth defects
  • Matatizo katika mfumo wa kuganda wa damu (clottaing disorders).
  • Mazoezi kupita kiasi (excessive exercise), afya iliyodhoofika (poor nutrition), matatizo ya kula (eating disoder).
  • Baadhi ya madawa au sumu.
  • Msongo wa mawazo (emotional stress)
  • Tatizo la kukosekana kwa usawa wa mfumo wa vichocheo mwilini (hormonal imbalance)
  • Uzito uliopitiliza (obesity)
  • Unywaji pombe kupindukia (heavy alcohol intake)
  • Magonjwa ya muda mrefu kama kisukari (diabetes)
  • Magonjwa ya kina mama (Pelvic inflammatory infection, PID)
  • Ovarian cysts and polycytic ovarian syndrome
  • Magonjwa ya zinaa (sexually transmitted disease, STD) au endometriosis
  • Saratani
  • Uvutaji sigara, madawa ya kulevya kama kokeni, bangi, hashishi nk.
  • Matatizo ya hedhi - wanawake wanaopata hedhi bila kutoa mayai (anovulatory menstrual cycle)
  • Kuwepo kwa cervical antigens ambazo huua shahawa za mwanamume na hivyo kusababisha kwa mwanamke kutopata ujauzito.

Tatizo la ugumba - linaweza kutokea kwa mwanamume wakati wa;
  • Kupungua idadi ya shahawa (decrease number of sperm)
  • Shahawa kuzuiwa kutolewa (blockage of sperm)
  • Shahawa ambazo hazifanyi kazi yake vizuri.
  • Kwa mwanamume, tatizo la ugumba husababishwa na;
  • Mazingira yaliyo na kemikali zinazoathiri uwezo wa mwanaume kumbebesha mimba mwanamke (environment pollutants)
  • Kukaa sehemu zenye joto kali sana kwa muda mrefu (exposure to high heat)
  • Matatizo kwenye mfumo wa viashiria vya asili (genetic abnormalities)
  • Unywaji pombe kupindukia, matumizi ya madawa ya kulevya kama kokeni, bangi, hashishi nk, hupunguza idadi na kiwango (quality) cha shahawa .
  • Kuzeeka (older age)
  • Kutumia dawa za vichocheo vya mwilini (hormonal supplements) ama kukosekana kwa baadhi ya vichocheo mwilini (hormonal deficiency)
  • Kuasiliwa (impotance)
  • Magonjwa ya korodani (testicular infections) au kwenye mishipa ya korodani (epididymis)
  • Historia ya matumizi ya baadhi ya dawa za saratani
  • Magonjwa ya zinaa (STD), ajali (trauma) au upasuaji
  • Historia ya mionzi (radiation exposure)
  • Retrograde ejaculation (matatizo ya kukojoa au kutoa shahawa)
  • Msongo wa mawazo (emotional stress)
  • Uvutaji sigara
  • Matumizi ya baadhi ya dawa kama cimetidine, spironolactone, nitrofurantoin.
  • Varicocele
  • Mumps
Viashiria na vipimo vya ugumba (infertility)
Kwa wanaume;

  • Semen analysis - Kipimo hiki kinahusisha uchukuaji wa shahawa kutoka kwa mwanamume ambaye amekaa siku 2-3 bila kujamiana na kuzipima kujua wingi, kiwango chake, shepu zake, viscosity of semen, motility and swimming speed.
  • Testicular biopsy - Kipimo cha korodani

Kwa wanawake;
  • Kipimo cha kiwango cha vichocheo kwenye damu (blood hormone levels)
  • Cervical mucus detection - Kipimo cha kuangalia kamasi za kwenye shingo ya kizazi ili kupima jinsi zinavyovutika (stretch), na kama ni za majimaji (wet) wakati wa mzunguko wa hedhi, na kama zina utelezi ambao huusishwa naovulatory phase
  • Kipimo cha kiwango cha joto mwilini (body basal temperature) - Kuongezeka kwa kiwango cha joto kwa 1 degree kutoka kiwango cha joto cha kawaida cha binadamu (37 C) kinahusishwa na ovulation ambapo mwanamke ana asilimia kubwa ya kushika ujauzito au yai limetolewa na ovaries.
  • Postcoital testing - Kupima kamasi za shingo ya kizazi (cervical mucus) zilizochukuliwa masaa 2-8 baada ya wapenzi kujamiana ili kuangalia mwiingiliano wa shahawa na kamasi za shingo ya kizazi.
  • Kipimo cha kichocheo aina ya progesterone kwenye damu (serum progesterone testing)
  • Kipimo cha ukuta wa uterus (biopsy of uterine lining or endometrium)
  • Kupima kichocheo aina ya Luteinizing hormone kwenye mkojo ili kuweza kutabiri lini yai litatolewa na ovaries ili kupangilia siku za kujamiana kwa wapenzi.
  • Hysterosalpingography (HSG) - Kipimo cha X-ray kinachotumia dawa maalum (contrast dye) inayoonyesha njia ya shahawa kutoka kwenye shingo ya kizazi kupitia ndani ya mfuko wa kizazi (uterus) na kwenye mirija ya uzazi(fallopian tubes).
  • Laparascopy - Direct visualization of pelvic cavity
  • Progestin challenge
  • Pelvic exam-hufanywa na daktari.
Tiba ya tatizo la ugumba (infertility)
Tiba ni kama ifuatavyo;
  • Ushauri nasaha na kuwaelimisha wapenzi wawili - Matatizo mengi ya ugumba hutokea kutokana na uelewa au ufahamu mdogo wa elimu ya uzazi na ya kujamiana kwa wapenzi au wanandoa.Kuna wanaume wengi ambao hufika kilele haraka wakati wa kujamiana na hivyo kutoa shahawa mapema (au kukojoa) kabla ya muda muafaka (premature ejaculation), hii husababisha kutopata ujauzito ambapo lawama zote hupelekwa kwa mwanamke pasipo mwanamume kugundua kuwa tatizo ni lake. Ifahamike kwamba hakuna muda uliotengwa ambao ni muafaka wa kufika kilele au kukojoa kwa mwanamume lakini watafiti wa mambo ya kujamiana wanashauri angalau mwanamume afike au akojoe baada ya dakika 15 na kuendelea. Hivyo ni bora kwa wapenzi kujiandaa kisaikolojia mwanzo na kuchezeana kabla ya kuanza kujamiana ili kurefusha muda kwa mwanamume.
  • Tatizo jengine ni kutofahamu lini hasa ni muda muafaka wa kujamiana ili kushika mimba kwa urahisi. Kuna wanawake ambao hawajui hata mzunguko wao wa hedhi (yaani hawajui wanaanza na kumaliza hedhi lini na wakati wa hedhi wanatumika kwa muda wa siku ngapi). Ongeza nafasi yako ya kushika ujauzito kwa kujamiana angalau mara 3 kwa wiki kuelekea wakati wa ovulation au kujamiana wakati wa kipindi chote cha ovulation. Ovulationhutokea wiki 2 kabla ya mzunguko wako mwengine wa hedhi, kama una mzunguko wa hedhi wa siku 28 (yaani kila baada ya siku 28 unapata hedhi), ni vizuri kujamiana angalau kwa siku 3 kati ya siku ya 7-18 baada ya kupata hedhi.
  • Kupunguza kunywa pombe kupindukia, kuvuta sigara, kuacha matumizi ya bangi, kokeni nk.
  • Kupunguza kiwango cha mazoezi kwa wanawake.
  • Kupunguza unene uliopitiliza
  • Kuwa na mpenzi mmoja mwaminifu kwani kuwa na wapenzi wengi huongeza athari ya kupata magonjwa ya zinaa.
  • Kuacha tabia ya kuvaa nguo nzito au zenye kuleta joto kali sehemu za siri kwa wanaume kwani joto kali sana hupunguza kiwango na kuathiri utolewaji wa shahawa.
  • Kula mlo kamili na wenye virutubisho vyote muhimu kwa afya njema.
  • Dawa za kutibu magonjwa kwenye mfumo wa uzazi, magonjwa ya zinaa nk.
  • Njia za kitaalamu za kupata ujauzito zijulikanazo kama in vitro fertilization na intrauterine fertilization.

Ugonjwa Wa Busha

09:44 Add Comment
Mabusha ni hali ya kujaa maji kwenye mfuko wa pumbu. Hali hii hutokea kunapokuwa na mkusanyiko wa maji kati ya tabaka mbili za utando unaozunguka korodani.

Inakadiriwa kuwa karibu asilimia moja ya wanaume wote kote duniani huathiriwa na tatizo hili. Kwa hapa nchini, tatizo hili ni maarufu sana maeneo ya mwambao wa Pwani ya Bahari ya Hindi, kiasi cha kuhusishwa na imani kadhaa.

Mojawapo ya dhana iliyozoeleka miongoni mwa watu wa mwambao ni kuwa mabusha yana uhusiano mkubwa na unywaji wa maji ya madafu. Aidha, tatizo hili limekuwa likichukuliwa na baadhi ya watu kuwa ni hali ya kudhalilisha ingawa kwa wengine huonekana ni hali ya kuwa ‘mzee wa heshima’ au ‘umwinyi’.
 Ifahamike pia kuwa, tatizo la mabusha halitokei kwa wanaume watu wazima tu. Watoto wa kiume hususani katika mwaka wa kwanza (infants) pia ni waathirika wakuu wa tatizo hili.
Kwa kawaida mabusha hayana maumivu na wala hayaleti madhara, isipokuwa kama yatapata uambukizi kwa sababu nyingine yeyote ile, hali inayowafanya wengi wa waathirika, hasa wa mwambao, kuwa wagumu kutafuta ufumbuzi wa tiba.
Hata hivyo, ni vyema kama mtu ana uvimbe wowote kwenye pumbu zake, kutafuta msaada wa kitabibu ili kuweza kuondoa uwezekano wa kuwepo kwa magonjwa mengine ya sehemu za siri kama vile saratani ya korodani (testicular cancer) n.k.

Mabusha husababishwa na nini?

Sababu za kutokea kwa mabusha hutofautiana kati ya watoto wa kiume na wanaume watu wazima.

Kwa watoto wa kiume
Kwa watoto wa kiume, mabusha huweza kuanza kutokea kipindi cha ujauzito.
Wakati wa ujauzito, korodani za mtoto wa kiume huwa kwenye tumbo lake kabla ya kushuka taratibu kuelekea kwenye mapumbu. Wakati wa ushukaji huo, kifuko kinachozunguka korodani kinachoitwa processus vaginalis hushuka sambamba na kurodani hizo na kufanya korodani kuzungukwa na maji.
Kwa kawaida, ndani ya muda wa mwaka mmoja, kifuko hiki hufunga na maji hayo yanayozunguka korodani yote hufyonzwa na kurudishwa kwenye tumbo la mtoto. Iwapo baada ya kifuko kufunga na maji yaliyomo kushindwa kufyonzwa kurudishwa kwenye tumbo la mtoto, mtoto hupata busha lijulikanalo kitaalamu kama busha lisilo na mawasiliano (non-communicating hydrocele).
Hali kadhalika, wakati mwingine inawezekana kifuko kikashindwa kufunga na hivyo maji yakaendelea kujaa ndani ya kifuko kuzunguka korodani. Aina hii ya mabusha kwa watoto ujulikana kama busha lenye mawasiliano (communicating hydrocele).

Kwa wanaume watu wazima

Kwa wanaume watu wazima, mabusha husababishwa na mambo makuu mawili; Kwanza, kitendo chochote kinachochochea tando zinazozunguka korodani kuzalisha maji kwa wingi kuliko kawaida, na njia ya pili ni kupungua kwa ufyonzaji wa maji yanayozunguka korodani kwa sababu ya kuziba kwa mirija ya lymph (blockage of scrotal lymphatic system) au kuziba kwa mishipa ya damu inayosafirisha damu kutoka kwenye pumbu kwenda sehemu nyingine za mwili (blockage of scrotal venous system).
Ongezeko la uzalishaji wa maji linaweza kutokana na Maambukizi au/na majeraha katika korodani (testicular inflammation au orchitis) au maambukizi katika mshipa ujulikanao kamaepididymis yanayoweza kusababishwa na kifua kikuu (tuberculosis) cha makende, au maambukizi yanayosababishwa na vimelea wafilaria (filariasis) wanaosababishwa na kuumwa na mbu aina ya Culex.
Kujinyonga kwa korodani (testicular torsion) kunakoweza kuzifanya korodani kutenda kazi zaidi ya kiwango chake (hyperactive testis).
Uvimbe katika korodani (testicular tumors) ambao husababisha uzalishaji wa maji kupita kiasi.

Kupungua kwa ufyonzaji wa maji hutokana na Kufanyiwa upasuaji kipindi cha siku za nyuma katika eneo la kinena, au operesheni ya upandikizaji figo ambazo zinaweza kuathiri mfumo wa lymph na vena na hivyo kupunguza ufyonzaji wa maji kutoka kwenye mapumbu.
Kuwahi kufanyiwa tiba ya mionzi kipindi cha nyuma nayo uhusishwa na kutokea kwa mabusha.

Kwa hapa kwetu Tanzania, kung’atwa na mbu aina ya Culex anayeeneza vimelea vya filaria kunaelezwa kuwa sababu kuu mojawapo inayopelekea kuwepo kwa tatizo la mabusha na matende hususani maeneo ya Pwani na mwambao.

Dalili za Mabusha
Katika hatua za awali, mabusha hayana dalili zozote (asymptomatic).
Hata hivyo, baada ya muda fulani, mapumbu hujaa na uvimbe huweza kuonekana hata kwa nje. Kwa kadiri uvimbe unavyozidi kuongezeka, dalili zifuatazo zaweza kujitokeza pia;
Muhusika kujihisi hali ya uzito na kuvuta sehemu za siri kutokana na kujaa na kuongezeka kwa uzito wa mapumbu.
Mgonjwa huweza kujihisi hali ya usumbufu na kutojisikia vizuri maeneo ya kinena mpaka mgongoni.
Kwa kawaida mabusha hayana maumivu yeyote. Hata hivyo, iwapo mgonjwa ataanza kujihisi maumivu, hiyo ni dalili ya kuwepo kwa uambukizi katika mshipa wa epididymis (acute epididymitis)

Uvimbe huwa na tabia ya kupungua iwapo mgonjwa atakaa kitako na huongezeka pindi anaposimama.
Iwapo mgonjwa atajisikia homa, kichefuchefu na kutapika, hizo ni dalili za kuwepo kwa uambukizi katika mabusha.
Kwa kawaida mabusha hayana muingiliano na uwezo na ufanisi wa utendaji wa ngono. Hata hivyo kuna taarifa tofauti za kitafiti kutoka bara Asia na Afrika Magharibi kuwa mabusha yanaweza kuathiri ufanisi wa ngono na kwa kiasi fulani kusababisha mhemko au msongo wa mawazo kwa muathirika.

Uchunguzi na Vipimo
Uchunguzi mzuri wa kitabibu (physical examination) huwezesha kugundua uwepo wa mabusha kwa kiasi kikubwa bila hata kuhitaji vipimo vya ziada. Vipimo uhitajika tu kwa ajili ya kuchunguza chanzo cha mabusha, madhara yaliyoletwa na mabusha au kujua hali ya korodani.
Vipimo ni pamoja na
Kupima damu (Full Blood Count) na mkojo (Urine Analysis) kuchunguza uwepo wa maambukizi kama vile vimelea wa filaria na mengineyo.
Ultrasound ya kinena pamoja na mapumbu: Aina hii ya kipimo hufanywa ili kuchunguza uwepo wa matatizo mengine tofauti na mabusha. Matatizo hayo ni kama vile ngiri, uvimbe, kujinyonga kwa korodani (testicular torsion), majeraha katika korodani, damu kuvuja kwenye kwenye korodani (traumatic hemorrhage) au maambukizi.

Matibabu ya Mabusha
Kwa watoto wadogo, kwa kawaida mabusha hupotea yenyewe ndani ya mwaka mmoja. Iwapo hayajapotea, mtoto uhitaji kufanyiwa upasuaji kama tiba.
Kwa wanaume watu wazima, mabusha pia huweza kupona yenyewe bila kuhitaji tiba. Iwapo mabusha hayajapotea na yanamletea mgonjwa usumbufu (discomfort) au hali mbaya ya kiumbo (disfigurement) hayana budi kufanyiwa upasuaji ili kuyaondoa.
Njia za tiba ni
Upasuaji: Upasuaji wa mabusha huweza kufanyika bila ya mgonjwa kuhitaji kulazwa (outpatient). Madhara yanayoweza kutokea wakati wa upasuaji wa mabusha ni pamoja na damu kuganda (blood clots), maambukizi au majeraha kwenye korodani. Hii ndiyo njia maarufu zaidi na ya kuaminika ya matibabu ya mabusha duniani kote.
Kunyonya maji kwa kutumia sindano maalum (Needle aspiration): Njia nyingine inayotumika kutibu mabusha ni kuyanyonya maji kwa kutumia sindano maalum (needle aspiration). Hata hivyo njia hii haitumiki sana sehemu nyingi duniani kwa sasa kwa sababu maji ya mabusha huwa yana tabia ya kujirudia baada ya muda mfupi hata kama yatanyonywa.
Baadhi ya matabibu hupendelea kudunga dawa maalum za kuzuia maji yasijae tena (sclerosing agents) mara baada ya kunyonya na kuyaondoa maji yote.
Njia hii ya kunyonya maji ya mabusha, hufaa zaidi kwa wagonjwa wasioweza kuhimili upasuaji. Madhara yanayoweza kusababishwa na tiba ya namna hii ni pamoja na maambukizi na maumivu kwenye korodani.
Hata hivyo wakati mwingine, bila kujali ni tiba gani imetumika, mabusha huweza kujirudia baada ya matibabu.

Madhara ya Mabusha
Kwa kawaida mabusha hayana madhara yeyote. Aidha mabusha hayawezi kuathiri uwezo wa mtu kuzaa. Hata hivyo mabusha yanaweza kuleta madhara iwapo tu kama yakiambatana na magonjwa mengine kwenye korodani.
Kwa mfano, kama mabusha yataambatana na maambukizi (testicular infection) au uvimbe kwenye korodani (testicular tumor), yanaweza kusababisha kupungua kwa uzalishaji na utendaji kazi wa mbegu za kiume (sperms) na kupelekea tatizo la ugumba kwa wanaume.
Hali kadhalika, iwapo sehemu ya utumbo mkubwa au mdogo imebanwa katika upenyo fulani kwenye sehemu ya ukuta wa tumbo, huweza kusababisha ngiri (strangulated hernia), hali ambayo ni hatari kama isipotibiwa haraka.